Jumatano , 6th Jul , 2016

Mwanasoka nyota wa timu ya taifa ya Argentina na Barcelona Lionel Messi amehukumiwa kifungo cha miezi 21 jela.

Mwanasoka nyota wa timu ya taifa ya Argentina na Barcelona Lionel Messi amehukumiwa kifungo cha miezi 21 jela kwa kosa la kukwepa kulipa kodi, vyombo vya habari vya Hispania vimesema.

Baba wa Messi, Jorge Messi naye pia amehukumiwa kifungo cha jela kwa kukwepa kodi katika taifa la Hispania ya kiasi cha dola za Marekani milioni 4.5.

Pia Messi na baba yake wanakabiliwa na faini ya mamilioni ya euro, kwa kuhifadhi fedha ili kukwepa kodi katika mataifa ya Belize na Uruguay.

Hata hivyo kunauwezekano wakaepuka kifungo cha jela, kutokana na mfumo wa sheria za Hispania kutoa fursa ya kuwa chini ya uangalizi wa mahakama kwa watu wa vifungo chini ya miaka miwili.