Jumatano , 8th Nov , 2023

Kiongozi msimamizi wa timu ya Mercedes Benz inayoshiriki mchezo wa kukimbiza magari Formula 1 Toto Wolff amesema gari walilotumia msimu huu wa 2023 halikubuniwa vizuri kwa ajili ya kushindana hivyo msimu ujao wa 2024 watakuja na gari jipya lenye ubunifu bira zaidi.

Kufuatia mwenendo mbaya wa Mercedez Benz msimu huu Toto wolff amesema gari lao msimu huu haliwezi kushindana kwa sababu linakosa ubora. Wolf amesema hayo baada ya kushuhudia madereva wake wakipata tabu na gari hilo kwenye mbio za Brazil Grand Prix.

Kwnye mbio za Brazil madereva wa timu hiyo George Russell na Lewis Hamilton walionekana wakipata tabu na gari ambapo Hamiliton alimaliza nafasi ya 8 kutoka nafasi ya 5 ambayo alianza wakati wa mbio zinaanza na George Russell alishindwa kumaliza mbio hizo baada ya gari kupata shida ya kiufundi.

Kwa ujumla msimu huu 2023 kwenye mbio 20 ambazo tayari zimefanyia Mercedes Benz ambao ndio mabingwa mara 9 wa Dunia hawajashinda mbio hata moja msimu huu lakini Bosi wa timu hiyo (Team Principal) Toto wolff amesema watapambana kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mbio 2 zilizosalia za Las Vegas GP na zile za Abu Dhabi GP.