Jumanne , 12th Jul , 2016

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Hans van der Pluijm amesema klabu ya Medeama ya Ghana si timu ya kudharau na wanalazimika kujipanga kwenye mambo mengi sana ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi.

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Hans van der Pluijm.

Kikosi cha Yanga kitavaana na kikosi cha Medeama katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumamosi Julai 16 mwaka huu.

Kocha wa kikosi hicho raia wa Uholanzi ambaye makazi yake yako nchini Ghana, amesema wapinzani wao pia ni timu bora.

"Timu inayofika katika hatua hii, haiwezi kuwa timu ya kubahatisha, hatuwezi kuwadharau ndiyo maana tumekuwa na maandalizi ya juhudi kubwa"

"Tumeangalia makosa, tumeangalia vitu vya kuongeza na tunavifanyia kazi hakuna mjadala, tunataka kushinda na tunajua haiwezi kuwa rahisi", alisema Pluijm.

klabu ya Yanga iko kundi A na inashika mkia huku TP Mazembe ikiwa inaongoza na kufuatiwa na Mo Bejaia na Medeama.