Jumapili , 9th Nov , 2014

Hatimaye Klabu ya Simba ya DSM leo imevunja MWIKO wa kutopata ushindi katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2014/15 kwa kuitungua Ruvu Shooting bao 1-0.

Wachezaji wa Simba wakimpongeza Emmanuel Okwi baada ya kufunga bao pekee la ushindi

Hatimaye Klabu ya Simba ya DSM leo imevunja MWIKO wa kutopata ushindi katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2014/15 kwa kuitungua Ruvu Shooting bao 1-0.

Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Taifa Dar es Salaam, haikuwa kazi rahisi kwa Simba kupata ushindi, kwani licha ya kutawala sehemu kubwa ya mchezo, imewachukua hadi Dakika ya 77 kupata bao hilo pekee lililotiwa kimiani na mganda Emmanuel Okwi.

Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha Pointi 9 na kupanda hadi nafasi ya 7 ikiwa imecheza mechi 7, imefunga magoli 7, imefungwa magoli 6, Sare 6, kushinda 1 na haijapoteza mchezo hata mmoja.

Mchezo unaofuata itacheza Desemba 26 katika dimba la Taifa itakapoikaribisha Kagera Sugar.

Katika mchezo mwingine uliopigwa leo, maafande wa JKT Ruvu wameichapa Ndanda FC kutoka Mtwara mabao 2-0.

JKT Ruvu imefikisha pointi 10, na kukwea hadi nafasi ya 6 ikiiacha Ndanda FC katika nafasi ya

Baada ya michezo hiyo ya mzunguko wa 7, ligi kuu itasimama hadi Desemba 26 mwaka huu.

Tags: