Akiongea leo na East Africa Television msemaji wa klabu hiyo Clement Sanga, ameweka wazi kuwa mlinzi huyo wa kati anaendelea vizuri kwa takribani asilimia 80 anaweza kutumika katika mchezo huo mkali wa kesho.
''Owino amepona na anaendelea na mazoezi hapa Kaitaba, tunauhakika tutamtumia kwenye mchezo wa kesho kwasababu jeraha lake chini ya mdomo ambapo alishonwa nyuzi saba amepona vizuri'', amesema Sanga.
Nyota huyo wa zamani wa Simba SC ambaye ni raia wa Uganda aliumia kwa kuchanika chini ya mdomo kwenye mchezo wa ligi kati ya Mbeya City na Lipuli FC uliopigwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Owino alilazimika kushonwa nyuzi saba na sasa amepona.
Lipuli FC inashika nafasi ya tisa ikiwa na alama 15 baada ya michezo 14 huku wapinzani wao Kagera Sugar ikishika nafasi ya 14 ikiwa na alama 12 kwenye michezo 14.


