Alhamisi , 16th Jul , 2020

Mabingwa wa kihistoria wa michuano ya mpira wa kikapu ya Sprite Bball Kings inayoandaliwa na kituo cha East Africa Radio na Tv kwa udhamini wa kinywaji cha Sprite ,Mchenga Bball Stars wameingiza timu yao katika ligi daraja la kwanza msimu huu.

Mchenga Bball Stars baada ya kutwaa ubingwa wa Sprite Bball Kings msimu wa mwaka 2019.

Akizungumza na kipindi cha michezo cha Kipenga kinachoruka kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 2 hadi tatu usiku, kocha na muasisi wa timu hiyo Mohamed Yusuph amesema wameanza kushiriki ligi daraja la kwanza, na baadae watacheza RBA na kisha katika ligi ya Taifa huku wakiendelea kusuka vijana wenye uwezo wa juu ili waendelee kutawala michuano ya Sprite Bball Kings.

Mchenga iliandikisha historia ya kutawala michuano ya Sprite Bball Kings tangu kuanzishwa kwake mwaka 2017 ambapo imetwaa kombe kwa miaka yote mitatu pamoja na zawadi ya kitita cha shilingi miliono 10 za kitanzania.