Jumanne , 19th Mei , 2015

Michuano ya masumbwi klabu bingwa mkoa wa Dar es salaam iliyotarajiwa kufanyika Mei 25 mwaka huu imepelekwa mbele mpaka Juni 15 chama cha masumbwi mkoa wa Dar es aalaam DABA, kukumbwa na tatizo la ukata.

Akizungumza na East Africa Radio, mwenyekiti wa DABA, Godfrey Akolory amesema ukata unaoendelea kuwaandama katika chama hicho umepelekea kushindwa kununua vifaa vya masumbwi ambavyo ni muhimu katika mashindano hayo.

Akalort amesema, baada ya kuona siku zimebakia chache kabla ya kuanza kwa mashindano hayo, ndipo walipoamua kisogeza mbele hadi tarehe hiyo, ili kujiandaa na pia kutoa nafasi kwa mabondia kujinoa kikamilifu na kuweza kupata wachezaji wazuri watakaounda kikosi cha timu ya mkoa.

Mashindano hayo yanatarajia kushirikisha klabu 20 kutoka Dar es salaam ambapo baada ya hapo wataunda timu ya mabondia wenye uwezo kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Taifa.