Jumatano , 7th Feb , 2024

Kocha Mkuu wa Kikosi cha Mashujaa ya Kigoma Mohammed Bares amesema katika mchezo wao kesho dhidi Yanga Sc utakaochezwa majira ya saa moja katika Uwanja wa Azam Complez wataingia kwa tahadhari kubwa na kucheza kwa kuwaheshimu

Akizungumza na waandishi wa habari Leo jumatano ya Februari 7,2024 Kocha Baher amesema watambua wapinzani wao Yanga SC ni timu kubwa hivyo naaamini kwa maelezo ambayo nimeyatoa kwa wachezaji wangu tutaweza kupata ushindi.

“Tumejiandaa vizurii na tunatambua ni mchezo mkubwa ambao unatukutanisha na timu kubwa hivyo tumejipanga kucheza kwa malengo “amesema Bares

Katika msimamo wa Ligi kuu ya NBC Tanzania kikosi cha Yanga SC kinashika nafasi ya kwanza na ala zake 34 huku Mashujaa Fc ikishika nafasi ya mbili kutoka mwisho na alama zao 9.