Ijumaa , 22nd Mei , 2015

Mashindano ya wazi ya mchezo wa Gofu ya Northern Provice yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi hapo kesho viwanja vya Gymkhana jijini Arusha.

Akizungumza na East Africa Radio, Makamu Mwenyekiti wa chama cha Gofu nchini TGU, Joseph Tango amesema, mashindano hayo yatashirikisha vijana wachezaji wa jinsia zote kutoka klabu wenyeji Arusha, Gymkhana Dar es salaam, Lugalo, Morogoro, Misenyi, Kagera na mikoa mingine ambayo mpaka sasa imeahidi ushiriki lakini bado hazijahakiki majina ya vilabu.

Tango amesema, wanatarajia kuwa na changamoto ya kiushindani katika michuano hiyo kutokana na mashindano hayo kuwa ya wazi suala linalopelekea hata wachezaji wa viwango vya juu kushiriki michuano hiyo.

Tango amesema, mashindano hayo yatasaidia kuweza kupata vijana watakaounda timu nzuri ya Taifa itakayoweza kushiriki mashindano ya kimataifa hapo baadaye.