
Akizungumza na East Africa Radio, katibu mkuu wa RT, Suleiman Nyambui amesema, katika mbio za wazi kutashindanishwa wanariadha wa miruko, mitupo na mbio za viwanjani ikiwamo zile za kuruka vihunzi na kukanyaga maji ambazo kwa miaka mingi Tanzania ilizipa kisogo.
Nyambui amesema, wamelazimika kufanya michezo yote ya riadha ili kumpa kila mwanariadha fursa kuonesha kiwango chake kabla ya kuteua timu ya taifa.