Jumatano , 28th Oct , 2015

Chama cha Tenisi Tanzania TTA kimeandaa mashindano ya wazi ya mchezo huo kwa vijana walio chini ya miaka 18 yanayotarajiwa kuanza Novemba mwaka huu jijini Dar es salaam kwa kushirikisha timu za wanawake na wanaume.

Mmoja wa waandaaji ambaye pia ni kocha wa tenisi Salum Mvita amesema kuwa hivi sasa wapo katika harakati za kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kama ilivyopangwa.

Mvita amesema, kikubwa wanachotafuta ni fedha ili kuhakikisha wanafanikisha kila walichopanga ambapo wanahitaji kuhakikisha mpaka Desemba mwaka huu wawe wameshaandaa mashindano yasiyopungua matano.