Jumatatu , 24th Nov , 2014

Michuano ya Mpira wa Kikapu Taifa imeanza leo kwa kushirikisha mikoa nane kati ya mikoa zaidi ya 20 iliyoalikwa katika michuano hiyo.

Akizungumza na East Africa Radio,Kamishna wa Ufundi wa Chama cha Mpira wa Mikono nchini TBF,Manase Zabroni amesema michuano hiyo inasaidia kuinua vipaji kwa vijana walio katika vilabu mbalimbali nchini na pia kuweza kupata timu nzuri ya taifa itakayoweza kushiriki michuano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

Zabron amesema mashabiki na viongozi mbalimbali wanatakiwa kujitokeza ili kuweza kusaidia kuukuza mchezo huo hapa nchini na uweze kufanya vizuri katikia mashindano mbalimbali Duniani.