Ijumaa , 1st Jan , 2016

Mashabikiwa soka nchini wametakiwa kuendelea kuwaunga mkono wachezaji ili kuweza kuwapa nguvu ya kufanya vizuri zaidi.

Winga wa Klabu ya Yanga Simon Happygod Msuva amesema, bado wanasafari ndefu kwani bado wana mechi za kimataifa na yote ni kwa ajili ya kuitangaza nchi katika ramani ya soka.

Msuva amesema, kwa upande wao kwa mwaka huu wa 2016 wamejipanga vizuri na wanaamini watafanya vizuri kutokana na ushirikiano walionao pamoja na kuwashirikisha viongozi ili kuweza kutimiza malengo waliyojiwekea.