Ijumaa , 1st Jan , 2016

Nidhamu na kujituma ndiyo msingi mkubwa kwa vijana wa Tanzania wenye ndoto za kutaka kufika mbali kwenye mpira wa miguu,kama Nyota wa Tanzania na klabu ya TP Mazembe ya DR Congo Mbwana Samatta.

Nidhamu na kujituma ndiyo msingi mkubwa kwa vijana wa Tanzania wenye ndoto za kutaka kufika mbali kwenye mpira wa miguu,kama Nyota wa Tanzania na klabu ya TP Mazembe ya DR Congo Mbwana Samatta.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti hii leo jijini Dar es Salaam,shabiki wa soka Sudi Seif amesema kujituma kwaSamatta na kuchukulia mpira ni kazi,ndiyo kumemfikisha hapo alipo hii leo.

Naye shabiki mwingine wa soka Karim Sultan amesema Samatta alikuwa kama mwenye ndoto ya kufika mbali kwani alikuwa akiwahi kufika uwanjani kwa ajili ya mazoezi kabla ya wenzake,wakati anachezea Mbagala Market.

Amesema Samatta alikuwa akicheza soka kwenye mazingira magumu,lakini alijua nini ana tafuta na mungu amemsaidia hii leo.

Shabiki mwingine Pascal Maulelo amesema soka la Congo limemjenga Samatta kutokana na waamuzi wa huko wanachezesha kwa haki kuliko waamuzi wa Tanzania ambao baadhi yao wanashusha viwango vya wachezaji kwa kuzibeba timu.
Samatta aliyejiunga na mabingwa mara 5 wa Afrika TP Mazembe ya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akitokea klabu ya Simba ya Tanzania 2012,anatakiwa na klabu ya ligi kuu ya nchini Ubelgiji KRC Genk.

Kwa mujibu wa taarifa za wakala wa mchezaji huyo Jamali Kasongo,amesema Samatta atajiunga na timu hiyo ya Ubelgiji baada ya taratibu zote kukamilika.