Alhamisi , 19th Oct , 2023

Klabu ya Yanga imetozwa faini ya shilingi milioni 2 kwa kosa la mashabiki wake kurusha chupa za maji uwanjani mara baada ya timu ya Ihefu kufunga bao la pili, pia kwa kosa la maofisa wa benchi la ufundi wa Yanga kuonekana wakipinga maamuzi na kumzonga mwamuzi wa akiba.

Afisa habari wa klabu ya Yanga SC, Ally Kamwe ametozwa faini ya shilingi milioni 1 na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kosa la kumkejeli na kumdhalilisha mwamuzi, Tatu Malogo kupitia mitandao ya kijamii.

Imeelezwa kuwa, Kamwe alichapisha picha ya mwamuzi huyo katika ukurasa wake wa Instagram akiunganisha na wimbo wa Billnas uitwao ‘Maokoto,’ hali iliyotoa tafsiri ya kumhusisha mwamuzi huyo na masuala ya rushwa.