Jumatano , 7th Mar , 2018

Klabu ya soka ya SImba kupitia kwa msemaji wake Haji Manara imetoa utaratibu kwa mashabiki wake wanaotaka kusafiri na timu kwenda nchini Misri kwaajili ya mchezo wa marudiano na Al Masry.

Akiongea mbele ya wanahabari Manara amesema kuwa tayari klabu imeshafanya utafiti wa gharama ambazo mashabiki wanatakiwa kulipa ikiwemo gharama za usafiri kiasi cha Dola 500 zaidi ya shilingi milioni moja ambazo zitatumika kwaajili ya tiketi na Visa.

Manara pia ameongeza kuwa safari ya mashabiki inatarajiwa kufanyika ijumaa ya Machi 16 na watarejea Jumapili Machi 18 baada ya mechi kuchezwa Machi 17 siku ya Jumamosi.

Aidha Manara amesema kuwa baada ya emchi ya leo kuna timu ya watu itaondoka kuelekea Pwani ya Port Said huko Misry tayari kwa maandalizi ya kupata hoteli na usafiri kwaajili ya mashaniki watakaokwenda na timu.

Simba na Al Msry zinacheza leo mchezo wa kwanza Kombe la Shirikisho majira ya saa 12:00 jioni kwenye uwanja wa taifa na zitarudiana Machi 17 nchini Misri ili kupata mshindi wa jumla atakayefuzu hatua ya makundi.