
Martha ameweka wazi hilo ambapo amefafanua kuwa kilichotokea mpaka leo hizo taarifa zipo ni yeye kuishi kwa ndugu yake mmoja hapa jijini Dar es salaam lakini haikuwa kuwa kwaajili ya kufanya kazi za ndani.
''Sijawahi kufanya kazi za ndani ila nachokumbuka nilipokuja hapa Dar es salaam na mama yangu tukitokea Makambako nilianza kuishi kwa ndugu yetu kama mwaka mmoja hivi lakini haikuwa kwaajili ya kufanya kazi za ndani'', alisema.
Aidha Martha ambaye anatarajia kuachia album yake mpya hivi karibuni pia alisema hakuwahi kuacha shule ili aimbe kama ambavyo watu wengi wamekuwa wakisema. ''Sijawahi kuacha shule na hata hivyo nilikuwa na umri mdogo wala sikuwaza kama nikiimba nitapata hela''.