Wanariadha wakishindana kwenye michezo ya Olimpiki inayoendelea nchini Ufaransa.
China inashika nafasi ya pili ikiwa inajumla ya medali 53 lakini wanalingana idadi sawa ya medali za dhahabu na Marekani 21. Wenyeji wa michezo hii Ufaransa wapo nafasi ya tatu wameshinda medali 48, huku medali 13 ni dhahabu.
Tanzania pia inawawakilishi saba kwenye michezo hii ya Olimpiki lakini mpaka sasa bado hatujashinda medali hata moja. Ni mataifa 66 tu ndio yaliyoshinda medali mpaka sasa kati ya mataifa 206 yanashiriki michezo hii ya Olimpiki 2024.