
Mkwasa amesema, makocha wa vilabu mbalimbali wanatakiwa kuwaweka wachezaji katika viwango vizuri ili kuweza kupata wachezaji wakuongezea katika kikosi chake ambao wataweza kuipatia timu point tatu muhimu katika mechi dhidi ya Chad itakayofanyika Machi 25 mwaka huu ikiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Afcon zitakazofanyika 2017 nchini Gabon. .
Mkwasa amesema, makocha wa vilabu wanajukumu kubwa la kuwaandaa wachezaji kwani wao hawana muda mrefu wa kukaa na wachezaji kwa ajili ya kufanya nao maandalizi ya muda mrefu kutokana na muda mwingi kuwa katika vilabu vyao.
Taifa Stars itaanzia ugenini katika mchezo wake utakaopigwa Machi 25 mwaka huu Dar es salaam.