Jumatano , 13th Jun , 2018

Klabu ya Manchester United imetajwa na Jarida la Forbes kuwa ndio klabu ya soka yenye thamani kubwa zaidi duniani kwa mwaka wa pili mfululizo ikiwa imejitengezea mapato ya  dola bilioni 4.12, zaidi ya Trioni 9 kwa mwaka 2018.

Man United ambayo imemaliza msimu wa 2017/18 kwenye nafasi ya pili nyuma ya Manchester City ambao ni mabingwa imeendelea kuiburuza klabu ya Real Madrid ambayo kabla ya mwaka 2017 ilikuwa ikiongoza orodha hiyo kwa miaka minne mfululizo.

Forbes wamesema mapato ya Man United yameongezeka kwa asilimia 12 ukilinganisha na mwaka jana. Mabingwa wa Ulaya Real Madrid ambao jana wamemtangaza kciha wa Hispania Julen Lopetegui kuwa kocha wao mkuu, imeshika nafasi ya pili ikiwa na mapato ya dola bilioni 4.08.

Mabingwa wa La Liga Barcelona wameshika nafasi ya tatu wakiwa wametengeneza mapato ya dola bilioni 4.06. Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wao wameshika nafasi ya 4 baada ya kutengeneza kiasi cha dola bilioni 3.06. Mabingwa wa England Manchester City wametengeza dola bilooni 2.47 wakishika nafasi ya 3.

Kwenye 10 bora jumla ya timu 6 za England zimeingia huku timu moja kutoka Serie A ya Italia, Juventus, nayo ikiiingia. Ligi kuu ya Ufaransa imeshindwa kuingiza timu hata moja kwenye kumi bora.

Timu 20

1. Manchester United ($4.12bn)
2. Real Madrid ($4.08bn)
3. Barcelona ($4.06bn)
4. Bayern Munich ($3.06bn)
5. Manchester City ($2.47bn)
6. Arsenal ($2.23bn)
7. Chelsea ($2.06bn)
8. Liverpool ($1.94bn)
9. Juventus ($1.47bn)
10. Tottenham Hotspur ($1.23bn)
11. Paris Saint-Germain ($971m)
12. Borussia Dortmund ($901m)
13. Atletico Madrid ($848m)
14. West Ham United ($754m)
15. Schalke ($707m)
16. Roma ($618m)
17. AC Milan ($612m)
18. Inter Milan ($606m)
19. Leicester City ($500m)
20. Napoli ($471m)