Kikosi cha JKT Ruvu
Afisa habari wa JKT Ruvu Vedasto Sajini amesema, Malale amechukua nafasi ya Abdallah Kibaden ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa benchi la ufundi ndani ya timu hiyo.
Sajini amesema, wameamua kumpangia majukumu mengine Kibaden kutokana na kuheshimu mchango wake na uzoefu katika soka la Tanzania.
JKT Ruvu inaendelea na mazoezi kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara utakaoanza Agosti 20 mwaka huu.



