Siku mbili baada ya kumalizika kwa mashindano ya kutafuta klabu bingwa wa taifa wa mpira wa kikapu nchini Tanzania, baadhi ya makocha waliokuwa wanazinoa timu zao katika michuano hiyo pamoja na wachezaji wamefurahishwa na juhudi za Uongozi wa shirikisho ulioingia madarakani hivi karibuni kwa kuongeza idadi ay timu zilizoshiriki michuano hiyo.
Makocha Joseph wa savio na Bakari wa timu ya Bandari ya jijini Tanga pamoja na Nahodha wa Savio, Roman Anania wamesema michuano ya mwaka huu imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na ushiriki wa timu nyingi katika michuano hiyo.
Wakati huo huo, Katibu mkuu wa Shirikisho la Mpira wa kikapu nchini TBF Salehe Zonga amesema wapo mbioni kuanza mchakato wa kutafuta vijana watakaoshiriki katika michuano mbalimbali ya kimataifa yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni jijini Kampala nchini Uganda.