Jumatatu , 13th Jul , 2015

Timu ya Soka ya Majimaji ya Mjini Songea imepania kufanya makubwa katika msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi ujao.

Katika taarifa yake, kocha mkuu wa kikosi hicho, Hassan Banyai amesema, kikosi chake kinafanya mazoezi ya nguvu ili kujiweka tofauti na kuleta ushindani katika ligi hiyo.

Majimaji ilipanda daraja kushiriki ligi kuu soka Tanzania Bara msimu uliopita pamoja na timu za African Sports ya jijini Tanga, Mwadui FC ya Shinyanga na Toto African ya Mwanza.