Mshambuliaji kinda wa Liverpool Jordon Ibe akishangilia baada ya kufunga bao katika moja ya mechi za ligi kuu nchini Uingereza.
Bao pekee la ushindi la Liverpool limefungwa na mchezaji Jordon Ibe katika dakika ya 37 kipindi cha kwanza ushindi ambao umempa furaha kocha wake Jurgen Klopp na kumpa matumaini ya kutinga fainali ya michuano hiyo.
Licha ya kucheza vizuri Liverpool iliwapoteza nyota wake wawili muhimu Philipe Countinho na Mlinzi wa kati Dejan Lovren waliotoka kabla ya mechi kumalizika kutokana na kupata majeraha.
Kwa matokeo hayo sasa Liverpool huenda ikakutana kati ya Everton au Manchester City mchezo ambao utafanyika katika uwanja wa Wembley.
Mchezo mwingine wa nusu fainali ya kwanza unatarajia kupigwa usiku wa leo ambapo Everton watakuwa nyumbani Goodson Park kuonyeshana kazi na Mnchester city.







