Jumamosi , 18th Apr , 2015

Michuano ya soka kwa ligi ya wanawake mkoa wa Dar es salaam inatarajia kuanza kutimua vumbi hapo kesho kwa vilabu mbalimbali kuchuana vikali kuuwania ubingwa huo.

Kwa mujibu wa kamati ya mashindano ya chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA, maandalizi kuelekea michuano hiyo yamekamilika ikiwa ni pamoja na viongozi wa vilabu husika kupewa kanuni na taratibu zitakazotumika katika mashindano hayo.

Jumla ya vilabu nane vinatarajia kushiriki katika ligi hiyo ya wanawake, ambavyo ni Simba Queens, Real Tanzanite,Temeke Squad, Ever-Green Queens, JKT Queens, Lulu Queens, Mburahati Queens Na Uzuri Queens.

Mechi ya ufunguzi inatarajia kuzikutanisha timu za Temeke Squad dhidi ya Ever-Green Queens, itakayopigwa katika uwanja wa Mwalimu Nyerere Kinondoni jijini Dar es salaam.