
Lewis Hamilton ametetea taji lake la Monaco GP, baada ya kumshinda dereva wa Red Bull, Daniel Ricciardo kwenye mashindano ya Formula 1.
Miaka 8 baada ya kutafuta taji la Monaco mwaka uliopita na kushinda kutoka nyuma, Mwingereza Hamilton alitetea tena taji hilo na kuwa ushindi wake wa kwanza wa msimu na anampita Nico Rosberg kwa kuwa na pointi 24.
Rosberg, dereva mwenza wa Hamilton kwenye timu ya Mercedes alimaliza katika nafasi ya 7 baada kuwa na wakati mgumu.