Jumanne , 18th Jan , 2022

Mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich, Robert Lewandowski ameshinda tuzo ya Mchezaji bora wa Dunia kwa upande wa tuzo za FIFA The Best mwaka 2021 na kuwapiku Mohammed Salah (Liverpool) na Cristiano Ronaldo  (Man United).

(Baadhi ya washindi wa tuzo za FIFA The Best 2021)

Lewandowski ameshinda tuzo huyo baada ya jopo la wapiga kura wakiwemo Wanahabari za Michezo, manahodha na makocha wajumbe wa FIFA kumpigia kura nyingi kufuatia kufunga mabao 69 mengi zaidi tokea mwezi Agosti 2020 hadi Oktoba 2021.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Poland, sasa amewek arekodi ya kushinda tuzo hiyo mara mbili mfululizo sawa na mshambuliaji wa Manchester Unted, Cristiano Ronaldo aliyeshinda mwaka 2016 na 2017.

Kw aupande wa tuzo nyingine zilizotolewa kwenye hafla hiyo usiku wa jana ni pamoja na tuzo ya kocha bora wa mwaka ambapo Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel ameshinda baada ya kuwapa Chelsea ubingwa wa Ulaya msimu wa 2021.

Erick Lamela ameshinda tuzo ya goli bora la mwaka ‘FIFA Puskas Award’ alilolifunga alipokuwa Tottenham Hotspurs dhidi ya Arsenal kwa mtindo wa ‘Rabona’ huku Eduardo Mendy akitwaa tuzo ya Kipa bora wa Dunia.

Cristiano Ronaldo wa Manchester United amepewa tuzo Maalum ya heshima kwa kuwa mfungaji bora wa muda wote kwa upande wa timu za taifa kwa kufunga mabapo 115 na kumpiku Ali Daei wa Iran aliyefunga mabao 109.

Timu ya taifa ya Denmark imepata tuzo ya Mchezo wa Kiungwana ‘Fair Play’baada ya kushiriki kuokoa maisha ya mchezaji wake Christian Eriksen ambaye aliyezirai uwanjani baada ya kupata shambulio la moyo kwenye michuano ya UEFA EUROS 2021.

Alex Putellas wa Barcelona ameshinda tuzo ya nchezaji bora wa Dunia kwa Upande wa Wanawake, wakati Mashabiki wa Denmark na Finland wameshinda tuzo ya mashabiki bora