Jumamosi , 14th Mei , 2022

Klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani imethibitisha kuwa mshambuliaji wao Robert Lewandowski ameomba kuondoka klabu hapo. Mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo Hasan Salihamidzic amethibitisha.

Lewandowski amefunga mabao 49 katika michezo 45 kwenye mashindano yote msimu huu.

Lakini klabu hiyo imemtaka mshambuliaji huyo raia wa Poland mwenye umri wa miaka 33 amalize mkataba wake na The Bavarians unaomalizika Juni 2023. Msimu huu kwenye michuano yote Lewandowski amefunga mabao 49 katika michezo 45 kwenye mashindano yote.

Lewandowski ambaye ni mshindi mara mbili wa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia mwaka 2020 na 2021 alijiunga na Bayern mwaka 2014 akitokea Borussia Dortmund, na katika misimu 8 akiwa na klabu hiyo ameichezea jumla ya michezo 374 na kafunga mabao 343 ameshinda makombe 19 ikiwemo makombe 8 ya Ligi Kuu Ujerumani Bundesliga na moja la Ligi ya mabaingwa barani Ulaya.

Na amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu ya FC Barcelona ya nchini Hispania mwishoni mwa msimu huu.