Jumanne , 17th Jan , 2023

Nyota LeBron James amefunga alama 48 zikiwa ni alama nyingi kwake kufunga kwa msimu huu na kuisaidia timu yake Los Angeles Lakers kuwalaza Houston Rockets kwa alama 140 dhidi ya alama 132 kwenye mchezo wa ligi ya kikapu ya Marekani (NBA).

Mchezaji kikapu wa Los Angeles Lakers, LeBron James

LeBron mwenye miaka 38 sasa anafikisha alama 38,072 kwenye orodha ya ufungaji wa muda wote ndani NBA akiwa nyuma ya alama 315 za kinara wa ufungaji wa muda wote kwenye NBA Kareem Abdul-Jabbar.

Matokeo mengine,Boston Celtics imewalaza Charlotte Hornets kwa alama 130-118 huku nyota Jayson Tatum akifunga alama 51 kwa mara ya saba ndani ya msimu huu na kuchukua ribaundi 9 na kutoa pasi za usaidizi wa mabao mara 5 huku nyota Steph Curry ameisadia Golden State Warrior kuwalaza Washington Wizards kwa alama 127 dhidi ya 118 huku akifunga alama 41 na kuchukua ribaundi mara 7.