Mwalimu Ali Khamis Said wa Mchezo wa Kuogelea
Serikali na wadau mbalimbali wameombwa kujitokeza kuudhamini mchezo wa kuogelea hapa nchini ili uweze kutambulika na kuitambulisha nchi katika Dunia ya Michezo.
Akizungumza wakati wa kufunga kozi ya makocha wa mchezo wa kuogelea hapa nchini,Mkurugenzi wa Chama cha Kuogelea nchini (TSA) ambaye pia ni mratibu wa kozi hiyo,Marcelino Ngalioma amesema serikali na wadau mbalimbali wawekeze katika mchezo huu ambao kwa kiasi kikubwa unazidi kushuka kutokana na kukosa vifaa kwa ajili ya mafunzo na hata mazoezi kwa walimu na wanafunzi wa mchezo huo.
Ngalioma amesema katika mafunzo hayo yaliyoanza Juni 20 yaligharamikiwa na Chama cha kuogelea Duniani (FINA) ambapo kwa kuhakikisha wanauendeleza mchezo huu hapa nchini waliamua kutoa Mkufunzi kutoka nchini Uswiss Matthias Ludwing kwa ajili ya kuja kutoa mafunzo hayo yaliyohudhuriwa na makocha 22 kutoka mkoa wa Dar es salaam.




