Alhamisi , 8th Oct , 2015

Baraza la michezo tanzania BMT limetangaza kuwa uchaguzi wa chama cha mchezo wa kuogelea nchini utafanyika jumamosi hii ya octoba 10 mwaka huu mkoani morogoro.

Baraza la Michezo Tanzania BMT limetangaza kuwa uchaguzi wa chama cha mchezo wa kuogelea nchini TSA utafanyika jumamosi hii ya Octoba 10 mwaka huu mkoani morogoro.

Akizungumza hii leo Afisa habari wa BMT Najaha Bakari amesema kuwa taratibu zote zimeshakamilika ambapo nafasi zote zilizowekwa wazi kwa ajili ya wagombea zimeshapata watu hivyo wanasubiri siku ya uchaguzi ifike.

Najaha amesema usaili kwa ajili ya kuwachuja wagombea utafanyika siku hiyo hiyo asubuhi,na hakuna siku nyingine itakayopamgwa

Katika hatua nyingine Najaha amewataka wajumbe watakaoshiriki katika uchaguzi huo kupiga kura kwa viongozi wanaowaamini kuwa wataleta maendeleo katika mchezo huo hapa nchini.