
Europa League.
Katika kundi hilo, Genk imepangwa pamoja na timu ya Besiktas ya nchini Uturuki, Malmo ya Sweden pamoja na Sarpsborg 08 ya nchini Norway, ambapo mechi hizo zitachezwa kuanzia, 20 Septemba mwaka huu.
Kabla ya kuingia katika hatua hiyo ya makundi, Genk imecheza jumla ya michezo sita ya kufuzu ambapo imefanikiwa kushinda katika michezo yake yote.
Kiwango cha Mbwana Samatta kimeendelea kuwa bora katika klabu hiyo tangu aliporejea kutoka katika majeraha ya mguu, mpaka sasa amefunga jumla ya mabao tisa katika mechi sita za mwisho ambapo katika mechi mbili za mwisho za kufuzu hatua ya makundi ya Europa League amefunga mabao manne.
Genk inarejea katika hatua hiyo baada ya kuwa nje kwa miaka miwili ambapo mara ya mwisho kushiriki waliishia katika hatua ya robo fainali, baada ya kutolewa na klabu ya Celta Vigo ya Hispania ambayo nayo ilitolewa na mabingwa wa kombe hilo msimu wa 2016/17, Manchester United.