
Kipingu amesema, taarifa za awali za kusimamishwa kwa michezo ambayo kwa mwaka huu ilitakiwa kufanyika jijini Mwanza zilisema kuwa kulikuwa na mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu na walikubali kwa kutaka watafute mkoa mwingine lakini walishangaa kupata taarifa za matengenezo ya madawati.
Kipingu amesema, tangazo la kusimamisha kwa michezo lisingetakiwa kutangazwa haraka kiasi hicho na wasingeweka kuwa chanzo ni matengenezo ya madawati.
Kipingu amesema, ugonjwa wa kipindupindu ni uhalisia lakini matengenezo ya madawati ni zoezi endelevu ambalo halina uhakika wa kumalizika mara moja.
Kipingu amesema, kusimamisha michezo kwa wanafunzi inawaumiza wanafunzi wenyewe na ikizingatiwa tayari wanafunzi walikuwa njiani kuelekea Mwanza.
Kipingu amesema, shule, wilaya, mikoa na wadau waliojitolea kuunga mikono mashindano hayo yametumia gharama nyingi hivyo Serikali ilitakiwa kuwaita na kuongea nao kabla ya kufanya maamuzi.
Kipingu amesema, athari za kuahirishwa kwa michezo hiyo zinakwenda moja kwa moja kwa wanafunzi ambao mara nyingi wanaposhiriki mashindano na shule za nje ya nchi huwa wanajiona wameshashindwa kabla ya kumaliza mashindano.