
Konta (Kushoto), Serena (Kulia)
Konta mwenye umri wa miaka 25, sasa atakutana na kigogo wa tenesi Mmarekani, Serena Williams ambaye naye ameshinda 7-5 6-4 dhidi ya Barbora Strycova kutoka Jamhuri ya Czech.
Naye Mcroatia Mirjana Lucic-Baroni alimaliza kiu yake ya kusubiri kwa miaka 18 kutinga robo fainali kwa mashindano ya Gland Slam, baada ya kupata ushindi dhidi ya Mmarekani Jennifer Brady
Lucic-Baroni, mwenye umri wa miaka 34, alishinda kwa seti mbili za 6-4 6-2 na kutinga robo fainali kwa mara ya kwanza tangu atolewe na Steffi Graf kwenye mashindano ya Wimbledon mwaka 1999.