Jumatatu , 2nd Jan , 2017

Mchezaji namba moja wa tenisi nchini Uingereza, Johanna Konta ameanza vyema Mashindano ya Shenzhen Open kwa kumchapa Cagla Buyukakcay kwa seti za 6-2 6-0 mapema hii leo, nchini China.

Johanna Konta

Konta, anayeshika namba 10, kwa wachezaji bora wa kike duniani, alifunga alama tisa katika mchezo wake wa kwanza katika dakika ya 56.

"Nafurahia sana muda wangu mjini Shenzhen," Konta alisema.

Konta, mwenye umri wa miaka 25, ni Mwingereza wa kwanza Mwanamke, kuanza msimu kwenye 10 bora za tenisi, tangu, Jo Durie mnamo mwaka 1983.