
Luis Enrique - Kocha wa PSG
Mabingwa hao wa Ufaransa wameshinda mechi kumi mfululizo. Enrique ameionya Liverpool na akiutaja mchezo huo kuwa utakuwa "50-50".
"Inaonyesha kiwango chetu cha sasa, tunapaswa kufikiria kuhusu Ligi ya Mabingwa, mechi mbili dhidi ya Liverpool, tufikirie kuwa na njaa ya kushinda"
"Hatutabadilika sana ila itakuwa tofauti, itakuwa ngumu sana, bila shaka, lakini tuko katika kipindi bora zaidi cha msimu. Tutacheza dhidi ya timu bora zaidi ya Ulaya, iliyofuzu kwa ustadi, lakini haipo katika mawazo yetu kubahatisha, kukaa kwa kujilinda, tutashambulia na tutajaribu kufanya hivo"-Kocha Enrique wa PSG