Jumanne , 28th Jun , 2016

Kocha Roy Hodgson amejiuzulu kuifundisha timu ya taifa ya Uingereza baada ya kufungwa magoli 2-1 na Iceland na kutolewa nje ya michuano ya Euro 2016.

Kocha Roy Hodgson akitangaza kujiuzulu mbele ya waandishi wa habari.

Kocha huyo amekuwa akiinoa Uingereza kwa miaka minne baada ya kuchukua mikoba ya kocha Muitaliano Fabio Capello, lakini ameshinda michezo mitatu tu kati ya 11 ya michuano mikubwa.

Taifa la Iceland lenye idadi ya watu 330,000 tu, ni miongoni mwa taifa lililopo kwenye viwango vya chini kabisa vya soka katika michuano hiyo Ufaransa likiwa nafasi ya 34 duniani.