Alhamisi , 3rd Apr , 2014

Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), imeondoka nchini alfajiri ya hii leo ,ikiwa na matumaini makubwa ya kupata ushindi kwenye mechi dhidi ya Kenya itakayochezwa Jumapili (Aprili 6) katika mji wa Machakos.

Ngorongoro Heroes inafundishwa na kocha John Simkoko ambaye ameonyesha kuwa na matumaini na kikosi hicho kutokana na maandalizi aliyowapa na amewataka wachezaji wa timu hiyo kujitambua na kusema kuwa Tanzania ina wachezaji wengi wenye vipaji,

Lakini kinachomata ni maandalizi na kupata timu bora ya baadae kunahitaji maandalizi mazuri yanayotokana na mpango wa muda mrefu kitu ambacho kinahitajia uvumilivu na utayari ili kupata matokeo mazuri siku za usoni.