Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Kocha Nabi “Ninajua namna ya kuwakabili KMC”

Jumamosi , 16th Oct , 2021

Kocha wa klabu ya Yanga, Mtunusia Mohammed Nasreddine Nabi amesema anajua namna ya kuwakabili wapinzani wake klabu ya KMC ambayo wanataraji kucheza nayo Jumanne ya Oktoba 19, 2021 Songea Mjini, Mkoani Ruvuma.

(Kocha wa Yanga, Mohammed Nasreddine Nabi akiwa anatoa maelekezo mkwa mchezaji Feisal Salum wakiwamazoezini)

Nabi ameyasema hayo wakati kikosi chake kikiwa kinafanya maandalizi ya mwisho wikiendi hii kabla ya kusafiri leo Oktoba 16, 2021 kuelekea Mkoani Ruvuma.

Kocha huyo amesema, "Tunafanya mazoezi ya aina mbali mbali, kwa sasa tumezingatia zaidi kujenga stamina. Wachezaji wanatakiwa kuwa imara. Ligi ni safari ndefu, wanatakiwa wawe katika kiwango cha juu cha kushindana kuanzia mwanzo hadi mwisho wa msimu"

"KMC ni moja ya timu ambazo wachezaji wake wanatumia nguvu, ninajua namna ambavyo tutawakabili. Naamini tutapata kile ambacho tunakihitaji kama timu" Amesema Nabi.

Vile vile Nabi akagusia umuhimu wa kupata ushindi kwenye mchezo huo kwa kusema, "Tunahitaji ushindi katika mechi hiyo ili kutuweka kwenye nafasi nzuri, tukipata matokeo mazuri yatakuweka kwenye nafasi nzuri ya kuelekea katika maandalizi ya kuwakabili Azam, mechi zote zinahitaji kuwa na kikosi imara"

Yanga inataraji kujitupa dimbani siku ya Jumanne Oktoba 19, 2021 saa 10:00 jioni kwenye uwanja wa Maji Maji uliopo Songea Mjini, Mkoani Ruvuma kisha kurejea Dar es Salaam kujiandaa kucheza dhidi ya klabu ya Azam.

Baada ya michezo miwili ya Ligi kuu kuchezwa, Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na lama 6 baada ya kuwafunga Biashara United Mara na Kagera Sukari kwa 1-0 kwenye michezo hiyo ilhali KMC ni wa 15, wapili kutoka mkiani akiwa na alama 1.

HABARI ZAIDI

Coaster iliyoparamia nyumba Bukoba

Tisa wanusurika kifo Kagera

Picha ya Fat Joe na Chris Brown

"Chris Brown anafaa kuwa 2Pac wa kisasa" - Fat Joe

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji