Jumapili , 23rd Mar , 2014

Michuano ya klabu bingwa ya netball kwa vilabu vya nchi za Afrika Mashariki na kati iliyoanza hap

Michuano ya klabu bingwa ya netball kwa vilabu vya nchi za Afrika Mashariki na kati iliyoanza hapo jana imeendelea kushika kasi hii leo kwa michezo mbalimbali kucheza katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam ikihusisha timu za wanaume na wanawake

Mmoja wa makocha Ramadhan Zimbwe anayekinoa kikosi cha timu ya wanaume ya Polisi ya Zanzibar amesema mashindano ya safari hii yatakua magumu mno kutokana na timu nyingi kuonyesha ushindani mkubwa hali inayotokana na timu nyingi kufanya maandalizi mazuri.

Zimbwe amesema kuwa pamoja na hali hiyo timu yake imejipanga kuhakikisha inalibakiza kombe hilo hapa nchini.

Kwa.upande mwingine mkuu wa waamuzi Damiani Chonya ambaye anawasimamia waamuzi katika michuano hiyo amesema kuwa ikiwa ni siku ya pili tangu kufunguliwa kwa pazia la michuano hiyo hapo jana hali ya uamuzi imekua ni ya kuridhisha kwa kiasi kikubwa na hakuna malalamiko.

Chonya amesema malalamiko mengi ya maamuzi katika baadhi ya michezo ambayo imechezwa tangu jana na hii leo ni kutokana na baadhi ya wachezaji , viongozi wa vilabu na mashabiki kutofahamu vyema sheria za mchezo huo.
Aidha Chonya ametoa ushauri kwa viongozi wa vilabu, wachezaji na mashabiki kuuliza kwa mtu ambaye anajua vizuri sheria za mchezo huo badala ya kulalamikoa moja kwa moja maamuzi lakini pia akawataka waamuzi kuwa makini ili apatikane bingwa wa kweli na aliyestahili.