Jumapili , 26th Jul , 2020

Ratiba ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania bara inatarajia kuhitimishwa leo ambazo michezo yote itapigwa kwa muda mmoja katika viwanja tofauti tofauti.

Moja ya mechi ya Mtibwa Sugar na Mwadui FC

Michezo inayotarajia kuvuta hisia za wengi ni ile inayohusisha timu za Yanga na Azam FC pamoja na timu za Ndanda FC, Alliance FC, Mbeya City na Mbao ambazo zinapigania kupata nafasi ya kubakia ligi kuu au kucheza hatua ya mtoano kuipata nafasi hiyo.

Tanzania Prisons itacheza na Azam FC katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, Lipuli FC ikiwakaribisha Yanga katika Uwanja wa Samora mjini Iringa, Alliance ikiwa mwenyeji wa Namungo FC, Mbao FC dhidi ya Ndanda FC, KMC dhidi ya Mbeya City na Mtibwa Sugar dhidi ya Ruvu Shooting.

Yanga na Azam FC zinachuana kupata nafasi ya pili katika msimamo wa ligi huku kila mmoja akiwa na pointi 69 wakati huo timu zilizo mkiani mwa ligi ni pamoja na Singida United ambayo tayari imeshuka daraja, Ndanda FC, Alliance FC, Mbeya City, Mbao FC na Mtibwa.

Ratiba nzima ya mechi za leo ni hii hapa chini: