
Akizungumza na East Africa Radio, Mgeta amesema Ligi za Ujerumani zina majina ambapoinaanza Bundesliga, ikifuatiwa na Bundesliga ya pili na baada ya hapo ni Bundesliga ya nne na baada ya hapo unaingia Verbandsliga ambapo klabu aliyosaini inapochezea.
Mgeta amesema, anaamini kusaini kwake mkataba katika timu hiyom itakuwa daraja la kuendelea mbele zaidi katika soka na hana mpango wa kuongeza mkataba pale utakapomalizika katika klabu hiyo kwa anahitaji kwenda mbele zaidi.
Mgeta amesema anaamini akifika mbali zaidi kimataifa ataweza kuipeperusha bendera ya Tanzania katika ramani ya michezo na kuwataka vijana wenye lengo la kufika mbali zaidi katika soka kutumia nafasi watakazozipata.