Jumanne , 24th Nov , 2015

Timu ya Kilimanjaro Stars leo inatarajia kutupa karata yake ya Pili dhidi ya Rwanda katika michuano ya Chalenji katika mchezo wa makundi utakaopigwa Uwanja wa Awassa nchini Ethiopia.

Wakati Kill Stars ikikutana na Rwanda Zanzibar Heroes wataumana na Uganda ikiwa ni baada ya kufungwa na Burundi bao 1-0 katika mchezo wake wa kwanza uliochezwa wiki iliyopita uwanja wa Addis Ababa nchini humo.

Katika taarifa yake Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars Abdallah kibaden amesema, wachezaji wana ari kubwa ya kuibuka na ushindi ili kuweza kufikia malengo ya kuchukua Kombe hilo baada ya kulikosa kwa muda mrefu ambalo kwa sasa linashikiliwa na Kenya.

Kwa upande wake focha wa Zanzibar Heroes Hemed Morocco amesema, wana imani wataibuka na ushindi ili kujiwekea mazingira mazuri ya kuweza kusonga mbele katika michuano hiyo.

Kill Stars itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 4-0 dhidi ya Somalia ambapo mchezo wa leo watahitaji ushindi ili waweze kujihakikishia kutinga hatua ya robo fainali.