Jumanne , 20th Oct , 2015

Msimamizi wa kituo cha michezo kwa vijana kwa upande wa mchezo wa mpira wa kikapu Bahati Mgunda amesema wanatazamia kuwa na walimu wa mpira wa kikapu katika kila shule za msingi ambazo zitawakilisha katika mashindano ya vijana kati ya miaka 12 na 14.

Mgunda amesema, wiki hii na wiki ijayo watakuwa wakitembelea mashule ili kuhakikisha wanakuwa na mwalimu wa michezo atakayekuwa akiisimamia timu pamoja na kocha anayeuelewa mchezo huo huku kwa upande wao kama wasimamizi wakiandaa mafunzo mbalimbali za walimu na waamuzi ambapo vijana wanatakiwa kujitokeza kwa ajili ya kupata mafunzo ya kuwa waamuzi.

Mgunda amesema, kwa upande wa vijana washiriki wa mashindano watapata mafunzo kwa ajili ya kuelekea kwenye kambi ambayo hufanyika kila mwaka Afrika Kusini inayofahamika kama Basketball without Border Camps.