
(Mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfed Zaha)
(Wachezaji wa Arsenal wakihuzunika baada ya kufungwa na Crystal Palace)
Kichapo hicho kimewafanya washika mitutu hao wa london Arsenal kusalia katika nafasi ya 5 kwenye msimamo wa ligi kuu nchini England wakiwa na alama zao 54 sawa na majirani zao Tottenham hotspur walio nafasi ya 4 na lama 54 pia. Na hivyo sasa kufanya vita ya kuwania nafasi ya 4 kuahamia upande wa kaskazini mwa London kati ya Arsenal na Spurs, baada ya Manchester united kushuka hadi nafasi ya saba kufuatia sare dhidi ya Leicester Cityu siku ya jumamosi.
Mabao ya Crystal Palace yalifungwa na Jean Phillipe Mateta katika dakika ya 16, Jordan Ayew dakika ya 24 na wilfred Zaha aliyefunga kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 74 na kumfanya Zaha kuwa mchezaji watatu kwa wachezaji waliopewa penati nyingi zaidi katika historia ya ligi kuu ya Engalnd akipewa penati 18, anazidiwa na Jamie Vardy wa Leceister City aliyepewa penati 21, na Raheem Sterling aliyepewa penati 23.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho jumatano kwa mchezo mmoja ambapo Everton ya frank Lampard baada ya kupoteza michezo 7 katia ya 11 iliyopita itaenda kujiuliza ugenini dhidi ya Burnley mchezo utakao pigwa majira ya saa 3 na nusu usiku.