Alhamisi , 19th Nov , 2015

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania bara The Kilimanjaro Stars Abdallah Kibaden mputa amefafanua sababu ya kuteua wachezaji waliokuwa katika timu ya taifa iliyokuwa ikicheza mechi za kimataifa za kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2018 nchini urusi.

kibaden ambaye pia ni mshauri mkuu wa benchi la ufundi wa Taifa Stars amesema si rahisi kuunda kikosi kipya wakati mashindano ya chalenji yapo karibuni kuanza .

Kilimanjaro stars inatarajia kuondoka siku yoyote kuanzia kesho kwenda Ethiopia ambapo itaanza changamoto ya kuwania ubingwa wa michuano hiyo novemba 22 mwaka huu kwa kuumana na Somalia.

Timu hiyo ipo kundi moja na wenyeji wa michuano hiyo Ethiopia,Rwanda na somalia wakati zanziba heroes ambayo inaondoka leo ikipangwa katika kundi B lenye Bingwa Mtetezi Kenya, Burundi na Uganda .