
Kerr amesema anashangazwa na wachezaji wake kushindwa kupasia kamba wakati wanapobaki wao na golikipa kitu ambacho wamekuwa wakikifanyia kazi kila kukicha wanapokuwa kwenye mazoezi.
Kerr amesema, mshambuliaji wa kimataifa Paul Kiongera kutoka Kenya pamoja na mchezaji wa Azam Joseph Kimwaga anayecheza kwa mkopo Simba ndio wamemuangusha kwenye mchezo wa jana usiku kwani kabla hawajafunga goli la kwanza walipoteza nafasi nne ambapo Kimwaga alipoteza nafasi mbili za wazi, Kiongera akikosa goli akiwa umbali wa mita tatu kutoka golini.
Kerr amesema, wachezaji wengi a kikosi chake wamecheza zaidi ya mechi 20 ukijumlisha na mechi za timu ya taifa wengine wamecheza zaidi ya mechi 29 achilia mbali mechi za kirafiki za pre season hivyo kikosi alichokipanga ni kuweza kuwapa nafasi wachezaji ambao hawajapata nafasi ya kucheza ili waoneshe uwezo wao.
Licha ya kulazimishwa sare ya kufungana kwa magoli 2-2 na Jamhuri, kikosi cha Simba kilipoteza nafasi nyingi za kufunga za wazi kitu ambacho kimemkasirisha kocha Kerr.