Jumatano , 13th Apr , 2016

Vinara wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza klabu ya Leicester City imetoa wachezaji watatu katika orodha ya wachezaji sita wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa chama cha wanandinga wa kulipwa nchini Uingereza zitakazotolewa April 24 mwaka huu.

Jamie Vary(kulia)Riyad Mahrez(kati)Ng'olo Kante(kushoto)wakiwa katika picha ya pamoja.

Riyad Mahrez, Jamie Vardy na Ng'olo Kante wametajwa katika orodha hiyo wakiungana na mshambuliaji wa Totenham Hotspurs Hary Kane, kiungo wa West Ham United Dimitri Payet na kiungo wa Arsenal Mesuit Ozil.

Mahrez amekuwa na mchango mkubwa kwa klabu yake akiifungia mabao 16 na kutoa pasi za mabao 11 msimu huu wakati Vardy amefunga jumla ya mabao 21 katika Epl huku Ng'olo Kante amekuwa mhimili mkubwa wa eneno la kiungo wa kati wa Leicester City.

Kwa upande wake Hary Kane ameonesha makali yake akifunga mabao 22 na mpaka sasa ndiye kinara kwa ufungaji katika ligi, wakati Mesut Ozil ameingia kwenye orodha hiyo kwa mchango wake wa pasi 18 zilizozaa mabao kwa Arsenal huku Dimitri Payet akijumuishwa kwa kuhusika katika mabao 23 ya klabu yake akifunga mabao nane na na kutoa pasi 14 zilizozaa mabao katika mechi 24 alizocheza.

Katika hatua nyingine Hary Kane ameungana na wachezaji Delle Ali wa Spurs, Romelo Lukaku na Ross Barkley wote wa Everton, Mlinda Mlango Jack Butland wa Stoke City na Philipe Coutinho wa Liverpool kuwania tuzo ya mchezaji bora chipukizi msimu huu.