Jumanne , 17th Jan , 2023

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema kambi ya siku ya nane waliofanya Mjini Dubai imewapa mafanikio kwa kuwa Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amepata muda wa kukaa pamoja na wachezaji.

Ahmed amesema baada ya Robertinho kukaa na wachezaji amewasoma tabia zao za ndani na nje ya uwanja hivyo itakuwa faida kwake kuwaongoza katika mechi za mashindano.

“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumerejea salama jijini Dar es Salaam na kesho tutashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Mbeya City kwenye Ligi Kuu ya NBC.''

“Kambi yetu ilikuwa ya mafanikio mjini Dubai Kocha Robertinho amepata nafasi ya kukaa na wachezaji pia tumepata mechi nzuri za kirafiki ambazo zimetuonyesha mahali kikosi chetu kilipo kuelekea michuano iliyo mbele yetu,” amesema Ahmed.

kwa upande mwingine Msemaji huyo amesema  mechi mbili za kirafiki walizocheza zilikuwa kipimo kizuri kwao, kwa michuano ya ndani bali hadi Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo itaendelea mwezi ujao.