
Kally' Ongala
Msimu uliopita, Ongala aliyekuwa mshambuliaji nyota wa zamani wa Yanga ndiye aliyeisaidia Majimaji kubaki ligi kuu Bara kwa kufanya vizuri mwishoni mwa msimu.
Msimu huu Majimaji imeanza kwa kusuasua na tayari imepoteza mechi zote, jambo ambalo limewalazimu wadhamini wake wapya, kuhakikisha wanamrejesha kocha Ongala.
Mechi yake ya mwisho ya Ligi Kuu Bara, Majimaji imepokea kipigo cha mabao 4-0 Simba SC.